Mpango wa Malipo ya Ada – 2026

MalipoKiasi (Tsh)
Jumla ya Ada kwa Mwaka4,100,000/=
Awamu ya Kwanza – Januari1,025,000/=
Awamu ya Pili – Aprili1,025,000/=
Awamu ya Tatu – Julai1,025,000/=
Awamu ya Nne – Septemba1,025,000/=
Matibabu100,000/= kwa mwaka
Rimu ya Karatasi – Januari17,000/=
Rimu ya Karatasi – Julai17,000/=

Ada inaweza kulipwa kwa awamu nne sawa za Tsh 1,025,000/=.

Kwa Mwanafunzi Mpya

Mwanafunzi anayechagua kujiunga na shule kwa mara ya kwanza anatakiwa kufanya malipo ya awamu ya kwanza pamoja na gharama nyingine za kujiunga, ambazo ni:

  • Ada ya kujiandikisha: Tsh 150,000/=
  • Karo ya muhula wa kwanza: Tsh 1,000,000/=
  • Sare za shule: Tsh 410,000/=
  • Matibabu: Tsh 25,000/=
  • Kitambulisho: Tsh 10,000/=
  • Rimu ya karatasi: Tsh 17,000/=

Fomu ya kujiunga inaonyesha jumla ya malipo ya awali kuwa Tsh 1,612,000/=.

UNIFORM YA SHULE ZA SEKONDARI

Wanafunzi wote wa Sekondari wanatakiwa kuwa na sare kamili ya shule kama ifuatavyo:

Aina ya SareIdadiGharama
Sare ya DarasaniJozi 2TSh 100,000
Sare ya Siku ya IbadaJozi 1TSh 50,000
Sare ya Nje ya DarasaJozi 2TSh 100,000
Tracksuit + T-ShirtSeti 1TSh 70,000
SoksiJozi 2TSh 20,000
Sweta2TSh 60,000
Tai1TSh 10,000
Jumla ya SareTSh 410,000

Akaunti za Benki

BenkiNamba ya Akaunti
NMB Bank31806600311
CRDB Bank0150225212600
NBC Bank027103003733
Tanzania Commercial Bank230207000005

Baada ya kufanya malipo, risiti ya awali ya benki (Bank Pay-in Slip) inapaswa kuletwa shuleni ili kupata stakabadhi rasmi. Mwanafunzi anatakiwa kuwa amekamilisha malipo yanayohitajika kabla ya kupokelewa shuleni.